The House of Favourite Newspapers

 Esma Mpenzi Wake ‘Full’ Minyoosho!

ESMA, WAKATI watu wakisema Esma haendani na mpenzi wake wa sasa hadi kufikia hatua ya kumuita kibenteni, mrembo huyo ameendelea kutupia picha za kimalovee kuudhihirishia umma kwamba hata waseme nini, hatojali.

Kupitia sehemu ya Insta Story huko Instagram, Esma ametupia picha zinazomuonesha akiwa kwenye hisia kali za mapenzi baada ya kutandikwa busu moja matata sana na jamaa wake huyo ambaye ‘anatrendi’ naye kwa sasa.

“Wanyooshe bibi, warambishe ndimu vizabizabina wanaofuatilia penzi lako sisi yetu macho bwana nyie endeleeni kufanya yenu,” alichangia shabiki maandazi mmoja kwenye ukurasa wa Instagram.

Comments are closed.