Farid Uwezo Alivyochezea Kichapo kwa Kudokoa Maandazi

MSANII wa filamu na ‘Kameraman’ maarufu kwenye maandalizi ya tamthilia ya Kapuni na filamu mbalimbali za Kibongo, Farid Jamali ‘Farid Uwezo’ ameibuka na kutoa siri yake aliyokuwa ameificha siku nyingi kuwa wakati yupo mdogo, shangazi yake alikuwa akifanya biashara ya kuuza maandazi ambapo anapika jioni lakini yeye alikuwa akiyadokoa na kujikausha.

 

Akizungumza na Ijumaa Wikienda, Farid alisema anakumbuka siku moja alipata kipigo kikali kutoka kwa shangazi yake baada ya kufumwa akiwa amedokoa maandazi, kitendo alichokuwa akikifanya mara kwa mara na kujikausha.

 

“Unajua shangazi alikuwa akipika tu na kuyaweka chumbani mimi nakwenda nadokoa, kesho yake akija kuhesabu anakuta yamepungua, ilikuwa akiniuliza nakataa, siku moja ndio akaamua kunikagua na kugundua, mwisho nikasema ukweli ambapo nilipigwa sana,” alisema Farid.

STORI: HAMIDA HASSAN


Loading...

Toa comment