The House of Favourite Newspapers

FCS YAWAOMBA WATANZANIA KUSHIKAMANA

Mwanachama wa Bodi ya Wakurugenzi ya Foundation for Civil Society,  Nesia Mahenge akielezea kwa undani mambo yanayopatikana katika ripoti hiyo ya Utafiti wa Uhisani nchini Tanzania.
Baadhi ya washiriki wakifuatilia kwa umakini uchambuzi wa Ripoti ya uhisani Tanzania iliyozinduliwa na Foundation for Civil Society  jijini Dar es Salaam.
Mmoja wa  wachambuzi wa Ripoti ya Utafiti wa Uhisani Tanzania (katikati) akizungumza jambo.

 

Watanzania wametakiwa kuwa na moyo wa kutoa kwa kusaidiana wenyewe ndani ya jamii na hata katika kuendeleza huduma mbalimbali za kijamii ili kuweza kusaidia taifa kusonga mbele.

 

 

Hayo yamesemwa  jijini Dar es Salaam na Mwanachama wa Bodi ya Wakurugenzi ya (Foundation for Civil Society) Bi. Nesia Mahenge wakati wa uzinduzi wa riporti ya utafiti maalum kuhusu uhisani na utamaduni wa kujitolea ndani ya Tanzania.

Ripoti hiyo ilihusisha utafiti uliofanywa kati ya februari hadi Aprili na kuhusisha mashirika ya Foundation for Civil Society (FCS) kwa kushirikiana na Jukwaa la Uhisani Tanzania (Tanzania Philanthropy Forum) kwa lengo la kupata taarifa muhimu kuhusu hali ya uhisani au hali ya kujitolea kwa jamii nchini Tanzania.

 

 

Mwanachama wa bodi hiyo alisisitiza umuhimu wa mtu mmoja mmoja  pamoja na taasisi mbalimbali binafsi hususani zinazofanya kazi za kijamii kuendelea kujitolea katika miradi mbalimbali ya maendeleo na kuacha tabia ya kuisubiri serikali kufanya kila kitu.

 

 

Aliendelea kusisitiza kuwa ni vyema kushiriki katika shughuli mbalimbali za kuleta maendeleo ikiwa ni mojawapo ya njia nzuri ya kuisaidia serikali katika kuinua miradi kadhaa ikiwemo elimu, afya, ujenzi na siyo kwa kuwezesha kifedha tu lakini hata katika kusaidia kuleta wahisani watakao fanikisha zoezi hilo pia ni hatua kubwa.

 

 

“Lakini pia katika hali ya kujitolea kwa Tanzania uelekeo wake sio mbaya  kwani Watanzania wanaonyesha kuwa wana moyo wa kutoa kwa kusaidiana, lakini pia hata katika juhudi za kujiletea maendeleo kwa kusaidia huduma mbalimbali za kijamii hali inaonyesha bado tupo vizuri” alisema Nesia.

 

 

Bi. Nesia amewashauri wadau kutumia matokeo ya utafiti huo kama sehemu ya kubadilishana uzoefu katika tasnia nzima ya uhisani na kujitolea katika jamii na kuhamasisha umuhimu wa uhisani miongoni mwa jamii ya watoaji pia kuweka muongozo wa kuendeleza uhisani Tanzania.

 

Comments are closed.