Fei Toto Ajikabidhi Azam FC

KIUNGO tegemeo wa Yanga, Feisal Salum ‘Fei Toto’, amejikabidhi rasmi Azam FC, baada ya kusema klabu hiyo imekuwa ikimwinda kwa muda mrefu na kwamba yupo tayari kutua kama wataafi kiana na Yanga wanaommiliki kwa sasa.

 

Fei Toto alijiunga na Yanga msimu uliopita kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Singida United, ambapo tangu atue klabuni hapo, amekuwa ni mmoja wa wachezaji wenye mvuto mkubwa kwa mashabiki wake, hivyo kama ikitokea akachukuliwa na Azam, ataacha simanzi nzito kwao.

 

Akizungumza na Championi Ijumaa, Fei Toto alisema ni kweli Azam wamekuwa wakimfuatilia muda mrefu hivyo kwa kuwa msimu huu unaelekea ukingoni, yeye yupo tayari kutua Azam ikiwa watatimiza vigezo na masharti ya uhamisho kutoka Yanga.

 

“Sina tatizo la kujiunga na Azam maana wamekuwa wakinifuatilia kwa muda mrefu, lakini mbali na hilo mimi kama mchezaji siwezi kuchagua timu ya kuchezea, zaidi naangalia maisha yangu hasa kwa sasa ambapo umri wangu bado ni sahihi kutafuta maisha bora,” alisema.

 

Championi lilifanikiwa pia kuzungumza na msimamizi wake Mohamed Kombo juu ya sakata la kwenda Azam, ambaye alisema: “Suala la Fei Toto kutakiwa na Azam kwa sasa mimi bado halijanifi kia, ila ninachoweza kusema ni kwamba, tulikuwa tunasubiria ligi iishe ili twende naye nje ya nchi kwa ajili ya majaribio maana ana ofa tatu nchi tofautitofauti za Ulaya ikiwemo Uingereza.”

 

MTOTO AFANYIWA OPERERSHENI MARA SABA / ZAPELEKEA UPOFU


Loading...

Toa comment