The House of Favourite Newspapers

Fei Toto: Hersi Akiondoka Yanga Narudi Klabuni Hata Sasa Hivi

0

KIUNGO mshambuliaji wa Timu ya Yanga, Feisal Salum ‘Fei Toto’ leo akifanya mahojiano na kituo kimoja cha redio amesema “Kabla ya mgogoro kuanza, nilikuwa nampigia Ghalib Said Mohamed akawa hapokei simu wala kujibu SMS zangu, baada ya sakata ndipo akanipigia simu sikupokea kwa kuwa niliona ni dharau, mimi masikini sina kitu lakini usinidharau”

Ameongeza “Sio kwamba namkwepa Rais wa Klabu ya Yanga, Mhandisi Hersi Said, nilikutana naye uso kwa uso nikamwambia msimamo wangu, akaniambia nenda CAS”

Anasisitiza “Ikitokea Hersi Said kaondoka Yanga, mimi narudi Yanga sasa hivi, sina tatizo na klabu wala mashabiki wa Yanga”
“Kama Rais sio Hersi sasa hivi narudi Yanga, sina shida na Yanga akiondoka Rais narudi sina shida na Mashabiki najua wananipenda “- Feisal Salum

Kiungo #FeisalSalum amesema “Nilipitia magumu nikiwa #Yanga lakini sikuwahi kusema, ilipofika muda wa kusaini Mkataba huu wa sasa shida ikaongezeka, kupewa Fedha ya usajili ikawa tabu, mshahara nilikuwa napata lakini ni baada ya kusumbuliwa.”

Amesema hayo wakati akizungumza na Clouds FM akieleza “Niliambiwa nauza Mechi, niliwahi kulia Uwanjani lakini Watu hawakujua nalia nini. Kiongozi wangu ananitukana na kuniambia kama siwezi nitarudi kwetu Pemba, niliwaambia Familia wananiambia nivumilie.”

YANGA: TUNARUDI NA KOMBE, MAYELE APIGILIA MSUMARI wa MOTO/ SIMBA WAJA na MPANGO MPYA | KROSI

Leave A Reply