The House of Favourite Newspapers

Fiesta Msimu wa 2017 Wazinduliwa Rasmi

0
Kaimu Mkurugenzi wa Masoko wa Tigo, William Mpinga (katikati) akizungumza na wanahabari, kushoto ni Sebastian Maganga na kulia ni Mwakilishi wa Basata, Mrisho Mbisho.

LILE Tamasha la Fiesta ambalo huvutia umati mkubwa wa watu  kutoka sehemu mbalimbali  nchini, limezinduliwa rasmi leo jijini Dar es Salaam.

Tamasha hilo ambalo huandaliwa kila mwaka na Kampuni ya Prime Time Promotions, mwaka huu linatimiza miaka 16 tangu kuanzishwa kwake. Linatarajiwa kufanyika katika mikoa 15 ambapo Watanzania watapata burudani na elimu jinsi ya kukabiliana na changamoto za maisha.

Sebastian Maganga akizunguza na wanahabari.

Akizungumza katika uzinduzi huo uliofanyika makao mkuu ya Kampuni ya Tigo jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Kamati ya Fiesta, Sebastian Maganga alisema tamasha hilo safari hii litajulikana kwa jina la Tigo Fiesta 2017 Tumekusomaa.

Wanahabri wakifuatilia uzinduzi huo.

Alisema safari hii Fiesta msimu wa 2017 wamejipanga vilivyo kuhakikisha Watanzania wananufaika na tamasha hilo katika nyanja mbalimbali ikiwa ni pamoja na: kupata burudani na elimu ili kuhakikisha ubora wake wa miaka 15 iliyopita haupotei.

“Lakini pia baada ya uzinduzi huu, zoezi la usajili wa wasanii watakaoshiriki katika tamasha hilo unaanza mara moja na utachukua kama wiki mbili hivi, baada ya hapo ndipo itakapofahamika ni mkoa gani Tigo Fiesta 2017 Tumekosomaa itaanzia,” alisema Maganga.

NA: MWANDISHI WETU| GPL

Usipitwe na Matukio, Install ===>Global Publishers App

VARANGATI: Mgomo wa Daladala DAR Yasimama, Madereva Watoa Yamoyoni

Leave A Reply