The House of Favourite Newspapers

FT: TEAM SAMATTA 6-3 TEAM KIBA, KUTOKA UWANJA WA TAIFA

 

FT: Timu Samatta 6-3 Timu Kiba
Uwanja wa Taifa
Kipindi cha kwanza
Goal: Hassan Kessy dk ya 5
Goal: Samatta dk ya 16,40
Goal: Thomas Ulimwengu dk ya 38
Goal: Kelvin John dk 60
Goal: Shaban Chilunda dk ya 80

Goal: kwa timu Kiba dk ya 18, 68 Simon Msuva
Goal: Kwa timu Kiba dk ya 21 Meddie Kagere
Dakika ya 34 Juma Kaseja anaonyeshwa kadi ya njano kwa kumchezea rafu Ibrahim Ajibu

Mchezo kwa sasa uwanja wa Taifa wa kirafiki kati ya timu Kiba na timu Samatta umekamilika kwa timu Kiba kufungwa mabao 6-3.

Hassan Kessy dakika ya tano wa timu Samatta anafunga bao kwa mkwaju wa penalti baada ya mchezaji wa timu Samatta kuchezewa rafu eneo la hatari.


Mbwana Samatta dakika ya 16 anapachika bao la pili akimalizia pasi aliyopewa na Thomas Ulimwengu.

Simon Msuva anafunga bao kwanza kwa timu Kiba akimalizia pasi ya Ibrahimu Ajibu dakika ya 18.

Meddie Kagere anapachika bao la pili dakika ya 21 akimalizia pasi ya Said Ndemla baada ya kupokea pasi kwa Simon Msuva.

Ulimwengu anapachika bao la tatu dk ya 38 akimalizia pasi ya Samatta.

Samatta anafunga bao la nne akimalizia pasi ya Jery Santo dk ya 40.

Kelvin John anafunga bao la tano dakika ya 60 akimalizia pasi ya Amri Kiemba.

Simon Msuva anapachika bao la tatu kwa timu Kiba dakika ya 68 akimalizaia pasi ya Feisal Salum.

Abdu Kiba wa timu Kiba amekosa penalti mbili kwenye kikosi chake zote zikisababishwa na Mwinyi Kazimoto.

Comments are closed.