The House of Favourite Newspapers

FULL VIDEO: Wachezazi Walivyotunukiwa Mo Simba Awards 2019

Ni usiku wa tuzo za MO umefanyika katika Ukumbi wa Hyatt Regency, ambapo muwekezaji wa Klabu ya Simba, Mo Dewji, ametoa tuzo kwa wachezaji wa klabu hiyo katika vipengele tofauti tofauti.

Usiku huo umehudhuriwa na mastaa mbalimbali wa soka akiwemo Nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta, muigizaji Aunt Ezekiel, Mwanamitindo Hamisa Mobeto na wachezaji wote wa klabu ya Simba.

MO SIMBA AWARDS 2019

Tuzo ya Golikipa Bora wa Mwaka – Aishi Manula.

Tuzo ya Beki Bora wa Mwaka – Erasto Nyoni akiwapiku Shomari Kapombe na Pascal Wawa.

Tuzo ya Kiungo Bora wa Mwaka – James Kotei akiwapiku Jonas Mkude na Mzamiru Yasin.

Tuzo ya Mshambuliaji Bora wa Mwaka – John Bocco akiwashinda Meddie Kagere na Emmanuel Okwi.

Tuzo ya Mchezaji Bora Mdogo – Rashid Juma akiwapiku Adam Salamba na Paul Bukaba.

Tuzo ya Mchezaji Bora wa Kike – Mwanahamisi Omary ‘Gaucho’.

Tuzo ya Wachezaji – Erasto Nyoni (Chaguo la Wachezaji wenzake).

Tuzo ya Mfungaji Bora (Kiatu cha Dhahabu) – Meddie Kagere ambaye pia ndiye mfungaji bora wa ligi kuu msimu uliomalizika akiwa amefunga magoli 23.

Tuzo ya Heshima – Hazim Dewji.

Tuzo ya goli bora la msimu – Clatous Chama alilofungwa dhidi ya Nkana FC kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka – Meddie Kagere.

FULL VIDEO: TUZO Za MO DEWJI Katika Ukumbi wa HYATT REGENCY

Comments are closed.