Gofu Lugalo Wapania Ubingwa NMB CDF Cup 2019

Mchezaji wa timu ya Benki ya NMB Lukundo Toroka akipiga mpira wakati wa michauno ya gofu ya Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania (NMB CDF Cup 2019) yaliyodhaminiwa na benki hiyo.

MICHUANO ya Gofu ya Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania (NMB CDF Cup 2019), imeanza rasmi jana na inataarajiwa kufungwa leo kwenye Viwanja vya Lugalo, ambako timu ya Gofu Lugalo ambao ni wenyeji wakitamba kuwa watabakisha taji ili kutomuangusha Mkuu wa Majeshi.

 

NMB CDF Cup ni michuano inayoratibiwa na Klabu ya Gofu Lugalo na kudhaminiwa na Benki ya NMB, ambapo mwaka huu inawakutanisha washiriki zaidi ya 100, wakiwemo zaidi ya 20 wanaocheza gofu ya kulipwa.

 

Mashindano hayo huwa ni maalum kwa ajili ya kuadhimisha siku ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), ambayo hufanyika Septemba 1 ya kila mwaka, lakini kutokana na ufinyu wa ratiba michuano hiyo ya imeanza jana na atafungwa leo.

 

Akizungumza baada ya uzinduzi wa mashindano hayo jana, Mwenyekiti wa Timu ya Gofu Lugalo, Brigedia Jenerali Mstaafu, Michael Luwongo, alisema anawaamini nyota wanaounda timu yao na hawatokuwa na kisingizio iwapo watashindwa kubakisha taji la jumla.

 

“Tunapozungumzia klabu ya gofu Lugalo, hatuna mashaka na hatutakuwa na visingizio, nawaamini wachezaji wangu, hasa ukizingatia ni Kombe la Mkuu wa Majeshi na nyota wangu hawatotaka kumuangusha bosi wao kwa kukubali kombe lichukuliwe na mwingine,” alitamba Luwongo.

 

Aliongeza ya kwamba, Mnadhimu Mkuu wa Jeshi, Mohamed Yakubu ndiye atakayefunga michuano hiyo leo, akimuwakilisha Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania, Jenerali Venance Mabeyo, ambaye ametingwa na ratiba ya majukumu yake ya kitaifa.

Na mwandishi wetu


Loading...

Toa comment