The House of Favourite Newspapers

GOLDEN WARRIORS YAWABAMIZA CAVS 4-0, YATWAA UBINGWA NBA

Golden State Warriors wakiwa na ubingwa wao baada ya kuwafunga mechi mfululizo 4-0 Cleveland Cavaliers ya Le Bron James.

 

TIMU ya Golden State Warriors imetwaa ubingwa wa ligi ya mpira wa kikapu Marekani (NBA) baada ya kuendeleza ubabe dhidi ya wapinzani wao Cleveland Cavaliers kwa kuwashinda mechi mfululizo 4-0 baada ya kutoka na ushindi wa mwisho wa pointi 108-5.

Katika  mchezo wa kuamua uliopigwa asubuhi ya kuamkia leo, Stephen Curry alitupia mara 37 ambapo Kevin Durant alitupia mara 20.

Hatua hiyo imekuwa ya majonzi makubwa kwa Cavs ambao wamepoteza michezo yao minne ya mwisho dhidi ya Golden.  Vilevile, nyota wa Cavs, Le Bron James, ambaye huenda alicheza mhezo wake wa mwisho kwa timu hiyo, alifichua kwamba alicheza akiwa ana maumivu kwenye mkongo wake.

Nyota wa Cavs, Le Bron James akiwa hoi baada ya mechi.

 

Kutokana na Golden kucheza vyema, wachezaji wao waliokuwa benchi walianza kushangilia mapema, sekunde chache kabla ya mchezo kwisha, wakiwa na uhakika wa ushindi na kutwaa ubingwa.

Huenda ushindi huo pia ukamafanya LeBron kuondoka katika timu ya nyumbani kwao ili kwenda kutafuta makombe sehemu nyingine.

WARRIORS YAKARIBIA KUPATA UBINGWA DHIDI YA CAVS, YASHINDA GAME 3

GOLDEN STATE WANACHAPA TU, SASA NI 2-0

GAME 1: Golden Warriors Waichapa Cleveland Cavaliers 124-114

 

Comments are closed.