The House of Favourite Newspapers

HAKURIDHISHI FARAGHA ? JIFUNZE!

UZURI wa mapenzi ni kuridhishana. Kila mmoja ‘ainjoi’ kukutana na mwenzake, alifuarahie tendo katika hali ambayo hawezi kuwa na hamu ya mapenzi pale anapokuwa amemaliza tendo. Kinyume na hapo, kukiwa na tatizo katika upande mmoja, furaha ya tendo inaondoka. Mmoja kati ya wapendanao anakuwa na shauku ya tendo wakati mwingine hana. Kitakachofuata hapo ni yule ambaye hajaridhika kutafuta njia mbadala ili kupata tiba ya mapenzi. Kwa kizazi cha sasa, watu wengi sana wamekuwa wakiteswa na tatizo la kutoridhishwa au kutomridhisha mpenzi wake.

Mwanaume anaweza kuwa anataka kumridhisha mpenzi wake, lakini anashindwa au mwanamke anataka kumridhisha mpenzi wake, lakini inashindikana. Wanapokutana  faragha, kila mmoja anakuwa na nia njema kabisa kutaka kukamilisha tendo la ndoa, lakini kwa tatizo linakuwa kwa mmoja wao na kuwafanya washindwe kufurahia tendo.

Mmoja kati ya wampendao anakuwa anawahi kuridhika wakati mwenzake anakuwa bado hajafikia muda wa kuridhika. Hapa ndipo zinapoibuka zile kauli za ‘mwenzangu haniridhishi’, ‘mwenzangu amekuwa gogo’ na nyingine nyingi zinazofanana na hizo.

Yule ambaye  haridhishwi huwa anakuwa katika wakati mgumu. Kutokana na desturi ya watu kutopenda kuambiana ukweli hususan katika jambo hili ambalo wengi wanaamini ni la aibu, hubaki nalo moyoni na kuendelea kuumia. Anavumilia hadi inafika wakati anachoka. Kinachofauta hapo ni kusaka suluhu. Ndiyo wakati wa kuanza kuwatafuta marafiki tofautitofauti ambao wanaweza kumshauri vizuri au vibaya.

Wapo wanaoweza kumshauri kwamba afanye vitu fulanifulani ili aweze kufanikiwa, lakini wengine huweza kumshauri atafute mtu mwingine ambaye atamridhisha. Kutokana na kero anayoipata, ni rahisi tu kufanya uamuzi wa kujaribisha kwa mtu mwingine. Usaliti ndiyo unaanzia hapo. Amani inatoweka na baadaye ugomvi huibuka, hapo ndipo watu hufikia hatua ya kushindwa kuvumiliana na hatimaye kuachana.

NINI CHA KUFANYA?

Kinachotakiwa kufanyika suala kama hili linapotokea, kwanza ni kuzungumza na mwenzako. Kama unaona kuna kitu hakipo sawa kwa upande wako, mueleze mwenzako ili muweze kutafuta suluhu. Kama pia tatizo unaliona lipo kwa mwenzako, tumia lugha nzuri kumueleza ili muweze kupata suluhisho. Yawezekana tatizo ambalo upo au yuko nalo ni la kisanaa ya tendo. Tendo hili linapaswa kufanyika kwa sanaa na ubunifu ili muweze kwenda sawa.

Yawezekana mwenzako anakurupuka, kabla hajakuandaa yeye anakuwa tayari ameshafika mbali kifikra hivyo kujikuta anakuacha kwenye mataa. Jadilini kwa kuelezana nini kifanyike ili kila mmoja afurahie tendo. Elimu ya kujiandaa inabidi kila mmoja aifahamu. Ushirikiano wa kulifanya tendo liwe na mashamsham linatakiwa.

Ujue wapi mwenzako anapenda umguse zaidi na kwa namna gani. Ni vyema mkawekana wazi ili kila mmoja asiwe mgeni na mwenzake. Ukimya wakati mwingine ndiyo unasababisha matatizo ya wapendanao kutofautiana. Yawezekana ulilonalo au alilonalo mwenzako ni la kitabibu, waweza kumshauri akaenda kutibiwa hospitalini na likaisha.

Mueleze mwenzako, mtashauriana na kupata suluhu. Hakuna sababu ya kuhangaika kwa kutafuta suluhu ya kuridhishwa na mtu mwingine. Unaweza kufanya hivyo kumbe nako bado ukakutana na tatizo ni lingine. Utahamia kwa mwingine bila kujua kiini cha tatizo huenda ni wewe mwenyewe, matokeo yake yatakuwa ni yaleyale.

Mheshimu mwenzako. Mtunzie siri kwani faragha inahitaji siri. Mnapokuwa wawili, elezaneni ukweli. Mueleze akutekelezee nini ili wewe uridhike. Kama kweli mmepandana kwa dhati na mna ndoto ya kufika mbali, hakika mtashughulikia tatizo na kusonga mbele. Kwa leo tuishie hapa, tukutane wiki ijayo kwa mada nyingine nzuri! Waweza kunifuata kwenye mitandao yangu ya kijamii, Instagram na Facebook natumia Erick Evarist, Twiter natumia ENangal

Comments are closed.