The House of Favourite Newspapers
gunners X

Halmashauri ya Wilaya ya Igunga Yatangaza Ajira 4 za Mwandishi Mwendeha Ofisi

0

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga anawatangazia Watanzania wenye sifa kuomba ajira za nafasi nne (04) baada ya kupokea kibali kutoka Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala

Bora. Bonyeza hapa >>NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA IGUNGA


1.0 MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA LA II

Idadi ya Nafasi: 04

1.1 MAJUKUMU NA KAZI

Mwajiriwa atakuwa na jukumu la:

  1. Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida na za siri.

  2. Kupokea wageni, kuwasaidia na kuwaelekeza sehemu husika.

  3. Kutunza kumbukumbu za matukio, miadi, wageni, vikao, safari na ratiba za kazi za Mkuu wake.

  4. Kutafuta majalada na nyaraka zinazohitajika katika utekelezaji wa majukumu.

  5. Kupokea na kusambaza majalada kwa Maafisa wa Idara/Vitengo husika.

  6. Kukusanya, kutunza na kurekebisha majalada na nyaraka.

  7. Kuandaa dondoo na maandalizi ya vikao mbalimbali.

  8. Kuandaa orodha ya mahitaji ya vifaa vya ofisi.

  9. Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na msimamizi wake.


1.2 SIFA ZA MWOMBAJI

Mwombaji anapaswa kuwa:

  • Mhitimu wa Kidato cha Nne (Form IV) au Kidato cha Sita (Form VI).

  • Mwenye Stashahada (Diploma) ya Uhazili au Cheti cha NTA Level 6 ya Uhazili kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali.

  • Amefaulu Hatimkato ya Kiswahili na Kiingereza kwa kasi ya maneno 100 kwa dakika moja.

  • Mwenye ujuzi wa matumizi ya programu za kompyuta za ofisi kama: Word, Excel, PowerPoint, Internet, E-mail na Publisher.


1.3 NGAZI YA MSHAHARA

  • TGS C


2.0 MASHARTI YA JUMLA

  1. Mwombaji awe Raia wa Tanzania mwenye umri wa miaka 18–45.

  2. Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kuomba na wanapaswa kubainisha aina ya ulemavu kwenye mfumo wa ajira.

  3. Waombaji waambatanishe CV yenye anuani, namba za simu, barua pepe na majina ya waamuzi (referees) watatu.

  4. Provisional results, testimonials au statement of results HAVITAKUBALIWA.

  5. Cheti cha kuzaliwa kiwe kimehakikiwa na Mwanasheria/Wakili.

  6. Waombaji waliowahi kuachishwa Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kwa kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.

  7. Waombaji walioko kwenye Utumishi wa Umma wazingatie taratibu husika za uwasilishaji wa maombi.

  8. Vyeti vyote vya elimu na taaluma viwe vimehakikiwa na Mwanasheria/Wakili.

  9. Waombaji waliosoma nje ya nchi wahakikishe vyeti vimethibitishwa na NECTA, NECTVET au TCU.

  10. Kughushi taarifa au sifa kutachukuliwa hatua za kisheria.

  11. Barua ya maombi iandikwe kwa Kiswahili au Kiingereza.


3.0 JINSI YA KUOMBA

Mkurugenzi Mtendaji
Halmashauri ya Wilaya ya Igunga
S.L.P. 19
IGUNGA

📅 Mwisho wa kupokea maombi: 01 Januari, 2026


Imetolewa na:
MKURUGENZI MTENDAJI (W)
HALMASHAURI YA WILAYA YA IGUNGA

Leave A Reply