The House of Favourite Newspapers

Halotel yaja na Ninogeshe na Halopesa ya Nandy

Msanii chipukizi wa kike wa nyimbo za kizazi kipya (bongo fleva), Faustina Mfinanaga maarufu kama “Nandy” ambaye ni  balozi wa  kampeni za Halopesa (kulia) akifungua shampeni kama ishara ya uzinduzi huo.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Halotel, Mhina Semwenda (kushoto) akizungumza jambo.
Naibu Mkurugenzi wa Kampuni ya Halotel, Nguyen Van Son akizungumza jambo.

 

Kampuni ya mawasiliano ya Halotelimezindua kampeni kabambe ya “Ninogeshe na Halopesa” maalum kwa wateja wanaotumia huduma za Halopesa.

Kuanzia sasa, wateja wa Halopesa wataweza kutuma pesa bure Halopesa kwenda Halopesa muda wowote.

Kuzinduliwa kwa kampeni hiyo ni muendelezo wa azma ya kuboresha huduma za fedha kwa njia ya mtandao kwa wananchi wenye vipato tofauti.

Licha ya kuondoa gharama za miamala kwa wateja wanaotuma fedha kutoka Halotel kwenda Halotel, wateja wetu watapata nafuu wanapotuma fedha kutoka Halopesa kwenda mitandao mingine.

 

Kampeni hii ni maalum kwa wateja wote wa Halotel waliopo mjini na vijijini wanaotumia huduma zetu kwa miaka miwili sasa tangu tulipoingia sokoni ambao watanufaika zaidi kwa kuokoa fedha ambazo wangekatwa wanapotuma pesa. Fedha hizo sasa wataweza kuzitumia kukidhi mahitaji yao mengine.

 

 

Akizungumza na waandishi wa habari, Naibu Mkurugenzi wa Kampuni ya Halotel, Nguyen Van Son amesema kampeni hii ni hatua nyingine ya kuhakikisha wateja wanakuwa na wigo mkubwa kufurahia na kunufaika zaidi na huduma za Halopesa bila kuwa na wasiwasi wa makato kila wanapotuma pesa mahali popote na wakati wowote.

 

 

“Hii ni fursa nyingine kwetu kuongeza tabasamu na furaha kwa wateja wetu walioenea nchi nzima kwa kuwapa huduma za fedha iliyo madhubuti inayoendana na hali ya uchumi kuondokana na usumbufu ambao wangeupata kwa kutumia njia nyingine kutuma fedha. Sasa wataokoa makato ya kufanya miamala,” alisema Son.

Mkurugenzi huyo alibainisha kwamba licha ya kuondoa gharama katika kutuma fedha kutoka Halopesa kwenda Halopesa, wateja watapata muda wa maongezi bure kila wanapoweka pesa kwa wakala.

 

“Habari njema tuliyonayo kwa wateja wetu ni kuendelea kuwanufaisha kila wanapotumia huduma ya Halopesa ambapo kwa sasa kila mteja atakaye weka pesa kwa wakala kuanzia shilingi elfu moja (1,000/=) atapata muda wa maongezi wa bure. Si hivyo tu wateja wetu wataendelea kunufaika kwa namna mbalimbali kila wanapotumia huduma za Halopesa,” alihitimisha Son.

 

Sambamba na uzinduzi wa kampeni ya Ninogeshe na Halopesa, kampuni ya Halotel imeingia makubaliano na msanii chipukizi wa kike wa nyimbo za kizazi kipya (bongo fleva), Faustina Mfinanaga maarufu kama “Nandy” kuwa balozi wake ambaye atahusika katika kampeni za Halopesa.

 

Hii ni hatua nyingine kwa msanii huyu kufanyakazi na Halotel na kuwakilisha huduma bora za mawasiliano inayotoa kwa mamilioni ya Watanzania nchi nzima.

 

Akizungumza katika hafla fupi ya kusaini mkataba na msanii huyo, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Halotel, Mhina Semwenda amesema kampuni imemchagua Nandy kwa sababu ana uwezo wa kuwa na mchango chanya utakaosaidia kukuza mauzo ya bidhaa na huduma, pamoja na kuimarisha jina la kampuni.

 

“Nandy ni msanii anayekonga nyoyo za mashabiki wake kupitia wimbo wake unaovuma kwa jina la ‘Ninogeshe’ na kumpa umaarufu unamfanya afahamike kwa watu wa rika zote. Unampa umaarufu ambao utasaidia kuiwakilisha vema kampuni ya Halotel,” alisema Semwenda.

 

Kwa upande wake, msanii wa bongofleva, Faustina Mfinanga  (Nandy) amesema hiyo ni fursa kubwa na ya kipekee kwake kuwa miongoni mwa familia ya kampuni hiyo na kupewa jukumu la kuiwakilisha ipasavyo kwa wateja wake na watanzania kwa ujumla kutokana na huduma bora za mawasiliano inazotoa.

 

Huduma ya Halopesa inatolewa na zaidi ya mawakala 55,000 wanawahudumia zaidi ya wateja milioni 1.5 walioenea nchi nzima.

 

Comments are closed.