The House of Favourite Newspapers

Harmo Awafutia Kesi Kajala na Paula

0
Paula Kajala

HATIMAYEstaa wa Bongo Fleva, Rajab Abdul ‘Harmonize’, amefuta kesi aliyokuwa amemfungulia mpenzi wake wa zamani, Kajala Masanja pamoja na binti yake, Paula Paul au Paula Kajala kwa tuhuma za kusambaza picha na video zake chafu, IJUMAA lina stori ‘exclusive’.

 

Aprili 20, mwaka huu, mwanamama Kajala ambaye ni staa wa Bongo Movies na mwanawe Paula walitiwa mbaroni kisha kuhojiwa kwa saa kadhaa na Jeshi la Polisi kabla ya kuachiwa kwa dhamana wakidaiwa kusambaza picha za utupu zilizodaiwa kuwa ni za Harmonize au Harmo ambaye ni C.E.O wa Lebo ya Konde Gang Music Worldwide.

 

HARMONIZE NA IJUMAA

Kwa mara ya kwanza tangu kutokea kwa sekeseke hilo, katika mahojiano maalum (exclusive interview) yaliyofanywa kati ya Gazeti la IJUMAA na Harmo mapema wiki hii jijini Dar, Harmonize alifunguka mambo mazito, lakini kubwa likiwa ni uamuzi alioufanya wa kuwasamehe Kajala na Paula na kufuta kesi hiyo.

 

“Sikia, binafsi nimeshaamua kuwasamehe Kajala na Paula, sitaki tena mambo ya kesi, nimeamua acha maisha mengine yaendelee,’’ alisema Harmo na kuongeza;“Namaanisha nimefuta kabisa kesi niliyokuwa nimewafungulia na sitaki tena kusikia mambo hayo,’’ alisema Harmo.

WATARUDIANA?

Hata hivyo, Gazeti la IJUMAA liliendelea kumchimba Harmo kama kwa sasa yupo tayari kurudiana na Kajala kwa kuwa amemsamehe, lakini hakutaka kuliweka wazi suala hilo.

 

“Mimi nimeshasema kuwa nimewasamehe, ndiyo maana hata kesi nimeamua kuitupilia mbali, sina shida na mtu na maisha mengine lazima yaendelee,’’ alisema Harmo ambaye alitengana na Kajala baada ya kudaiwa kumtaka kimapenzi Paula ili awe anakula kuku na mayai yake.

 

KESI ILIVYOKUWA

Aprili 20, 2021 aliyekuwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa ambaye kwa sasa amehamishiwa jijini Dodoma alithibitisha kukamatwa na kuachiwa kwa wawili hao baada ya kutua nchini wakitokea Dubai.

Kamanda huyo aliyataja makosa waliyotuhumiwa nayo kuwa ni kusambaza picha za utupu mitandaoni zinazodaiwa kuwa za Harmonize na msanii huyo ndiye aliyekuwa amefungua kesi hiyo baada ya kufikisha malalamiko yake Polisi katika Kitengo cha Makosa ya Mtandao.

 

Kwa mujibu wa Kamanda Mambosasa, wawili hao walikuwa wanaendelea kuripoti Polisi mpaka hapo jalada la upelelezi wa kesi yao litakapokamilika na kufikishwa mahakamani kwa kuwa kesi za aina hiyo huchukua muda mrefu kuzifanyia uchunguzi.

 

TUJIKUMBUSHE

Miezi kadhaa iliyopita, Harmo na Kajala waliingia kwenye mahaba mazito kiasi cha kuteka mitandao yote ya kijamii kwa kutupia mapichapicha kama yote.

 

Mara kadhaa, Harmo alipokuwa akihojiwa na Gazeti la IJUMAA, alikiri kumpenda Kajala mpaka kufikia hatua ya kusema kuwa endapo atamuacha, basi siku moja atajiua!Lakini mwisho wa siku mambo hayakwenda kama yalivyopangwa kwani wawili hao walitengana kwa aibu kwa kosa la msanii huyo kudaiwa kumtaka kimapenzi mtoto wa staa huyo Paula, hali iliyowasikitisha watu wengi.

Stori: Memorise Richard, DAR

Leave A Reply