The House of Favourite Newspapers

Harmonize Ampongeza Diamond Kwa Kuiga Mtindo Wake Wakati Akichugua Mpenzi Mpya -Video

0
Bosi wa Lebo ya Konde Gang, Rajab Abdul Kahali.

Bosi wa Lebo ya Konde Gang, Rajab Abdul Kahali almaarufu Harmonize au Konde Boy anaonekana kupendezwa mno na anayedaiwa kuwa mpenzi mpya wa bosi wake wa zamani aliyegeuka kuwa hasimu yake mkuu kimuziki, Diamond Platnumz.
Hivi majuzi, kumekuwa na uvumi kwamba Diamond yuko kwenye mahusiano na mwimbaji wa Ghana, Fantana ambaye ni mshirika wake wa mapenzi katika filamu ya uhalisia ya Young, Famous and African kwenye jukwaa la mtandaoni la Netflix.
Fantana ni mwimbaji na mwanamitindo matata wa Ghana ambaye pia ni mmoja wa wahusika wa kipindi cha ukweli cha Young, Famous and African.
Hata hivyo, hana historia ya uhusiano na Diamond mbali na kuwa washiriki wa kipindi hicho.

Diamond Platnumz

Moja kati ya sifa za malkia huyo mwenye umri wa miaka 25 aliyekulia nchini Marekani ni makalio yake makubwa, ambayo Harmonize anaonekana kuvutiwa na kufurahishwa nayo.
Baada ya kusambaa kwa video na tetesi za Diamond kutoka na Fontana, habari hizo zimemfikia Harmonize ambaye ameshindwa kujizuia na kumpongeza bosi wake huyo wa zamani.
“Karibu kwenye genge kaka, makalio,” Harmonize alisema kwenye Instagram, maneno yaliyoonekana kumzungumzia Diamond.
Harmonize anafahamika kupendelea wanawake wenye makalio makubwa.
Wengi wa wapenzi wake wa zamani walikuwa na sifa hiyo.
Hivi majuzi alimtambulisha mwanasosholaiti wa Rwanda, Phiona almaarufu Yolo The Queen kama mpenzi wake mpya.

Mwimbaji wa Ghana, Fantana.

“Sawa, siko single tena nimechukuliwa tayari,” mwimbaji huyo alisema kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Instagram.
Phiona ambaye anasemekana kuwa mmoja wa wanasosholaiti waliofanikiwa zaidi nchini Rwanda na viunga vyake ameweza kuvutia hisia za watumiaji wengi wa mitandao kutokana na umbo maalum la mwili wake.
Mwanadada huyo mrembo amebarikiwa kuwa na mwili uliopinda na makalio makubwa ambayo wanaume wengi wanayatamani.
Yolo anajulikana zaidi kwa misemo yake ya kuvutia ‘Wake Pray Slay’ na ‘Tamu Kuliko Asali.’
Harmonize alimtambulisha kama mpenzi wake mpya takriban miezi mitano baada ya kutengana na muigizaji Kajala Masanja ambaye pia ana makalio makubwa na kiuno kilichochongwa vizuri na Muumba.
Ni tabia ya Harmonize kuchumbiana na wanawake wenye makalio makubwa na anaonekana kufurahishwa na Diamond kufuata nyayo zake.

STORI NA SIFAEL PAUL

KWA MARA ya KWANZA: HARMONIZE AMPONGEZA DIAMOND kwa KUIGA MTINDO WAKE WAKATI AKICHAGUA MPENZI MPYA

Leave A Reply