The House of Favourite Newspapers

Harmonize Atua Bongo, Amlipua Diamond, Aanika Ukweli -Video

0

MWANAMUZIKI Harmonize, leo Alhamisi, Novemba 18, 2021 amerejea nchini akitokea Marekani alipokwenda kufanya shoo zake baada ya kutua nchini amezungumza na wanahabari katika Uwanja wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere na kueleza sababu zilizosababisha yeye kuondoka katika Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB) iliyo chini ya Diamond Platnumz.

 

Kauli za Harmonize baada ya kutua Dar es Salaam;-

“Lengo langu ilikuwa ni kutafuta peace, mimi nilikuwa naamini jinsi uwekezaji unavyokuwa mkubwa na mafaniko yatakuwa makubwa, Konde Gang ilikuwa ni ndoto yangu lakini sikutegemea kuifanya hivi karibuni.

 

“Kulikuwa hakuna jinsi lazima niondoke (WCB), nilichofanya, ni kujiuliza mtu gani ambaye angeweza kuzungumza na bro, nikaona Boss Joe (Joseph Kusaga), alikuwa mshkaji wake wakati huo wanataka kufungua media.

“Nikamfuata na kumueleza ukweli kuwa kuna hiki na hiki, sikumficha.

 

“Mi niko straight, ukinichukia sawa, usitake leo nikupe fadhila wakati mwanzo ulikataa fadhila zangu,”

“Nikamwambia Boss Kusaga, akasema nimuonyeshe mkataba wangu, nikamuonyesha akasema mkataba huo una vitu vingi na hata akinitafutia mwanasheria siwezi kulipa fedha.

 

“Nikamwambia sitaki anitafute mwanasheria, kuna mambo mawili, aongee na bro tukayamalize au au nitafute njia ya kulipa fedha za kuvunja mkataba.

 

“Ninachotaka mimi ni amani, akasema atanirudia, ila hakunirudia, nikasema hapa nimekosa msaada.

 

“Nikamfuata mama yake Nasibu, mama Dangote, nikamueleza kuwa kuna vitu siridhiki navyo.

“Tumetoka mbali na bro, sikutaka kuondoka vibaya, nilitaka nimfanye yeye awe nguli wa muziki Afrika, afeel proud kunisainisha mimi.”

Leave A Reply