HAZARD, REAL MADRID MAMBO SAFI

Eden Hazard

REAL Madrid sasa wana uhakika kwamba Eden Hazard atasaini mkataba klabuni hapo mapema kabisa kabla ya kuanza kwa maandalizi ya msimu mpya.

 

Hazard amebakiza mwaka mmoja kumaliza mkataba Chelsea lakini anataka kuungana na kocha Zinedine Zidane pale Madrid.

 

Taarifa kwenye gazeti la Ufaransa la L’Equipe zinadai kuwa Chelsea na Real Madrid wameshakubaliana ada ya pauni milioni 87 (Sh bilioni 259.4).

 

Wamekubaliana kwamba Hazard atasaini mkataba baada ya fainali ya Ligi ya Europa, Mei 29. Chelsea wamegoma kuzungumza chochote kuhusiana na hilo lakini ni wazi kwamba sasa wanamruhusu Hazard aondoke. Pia wanaweza kumpoteza kinda Callum Hudson-Odoi, ambaye anatakiwa na Bayern Munich.


Loading...

Toa comment