The House of Favourite Newspapers

HECHE: Ziko Wapi Dola Milioni 500, Bora Wakoloni – VIDEO

Mbunge wa Jimbo la Tarime Vijijini, John Heche, akichangia hoja katika bajeti ya Wizara ya Maji na Umwagiliaj, amesema enzi za ukoloni kulikuwa na mabomba mengi ya maji mijini na vijijini tofauti na sasa ambapo tatizo la maji limeongezeka nchini.

Mbunge huyo amemhoji Waziri wa Maji, Eng. Kamwelwe kuhusu dola milioni 500 (sawa na Tsh. Trilioni 1.14)  ambazo wizara yake ilidai zimetolewa na Serikali ya India kwa ajili ya kusaidia miradi ya maji nchini.

Aidha, Heche amesema wakati wa ujenzi wa Ofisi za Mabasi ya Mwendokasi, Jangwani jijini Dar, mbunge John Mnyika aliishauri Serikali kuwa eneo hilo hujaa maji licha ya ushauri wake kutofanyiwa kazi jambo ambalo sasa Serikali imelazimika kufanya mazungumzo ili kuhamisha kituo hicho kukipeleka Stendi ya Ubungo kutokana na maji mengi kujaa wakati wa mvua kubwa.

 

Comments are closed.