visa

 Husna Maulid bora asile, kisa..!

MREMBO ambaye alishakwaa skendo mbalimbali za kupiga picha na kuachia mwili wake wazi, Husna Maulid amesema kutokana na kupenda urembo ni bora hata kushinda njaa lakini ahakikishe anavaa vizuri na kupendeza. Akibonga na Za Motomoto ya Risasi, Husna alisema kuwa anaweza kuwa na kiasi cha shilingi elfu 10,000 lakini akakutana na gauni zuri na ana njaa bora anunue apendeze hata akikaa bila kula siku nzima.

“Huwezi amini napenda sana urembo kuliko kitu chochote kile, napenda kupendeza sana na nikiwa na hela kidogo nahitaji kitu cha kupendeza mwilini mwangu,” alisema Husna.

Stori: Imelda Mtema
Toa comment