The House of Favourite Newspapers

Irene Uwoya Ammwagia Sifa AliKiba

Irene Uwoya akiwa ndani ya Club Next Door Arena iliyopo Masaki jijini Dar ambapo kulikuwa na Tamasha la Funga Mwaka lililoandaliwa na AliKiba na kundi lake.

MSANII wa filamu za Kibongo mwenye mvuto wa aina yake kwenye tasnia ya sinema za Kibongo, Irene Uwoya amesema kuwa anamkubali mwanamuziki AliKiba huku akitaja Wimbo wa Hadithi kuwa ndiyo wimbo wake pendwa wa muda wote.

 

Uwoya amefunguka hayo baada ya kuonekana kwenye tamasha la msanii huyo la kufunga mwakalililofanyika Club Next Door Arena iliyopo Masaki jijini Dar ambapo amesema kuwa hajawahi kuonekana akiwa karibu na Kiba lakini ni mtu anayeikubali kazi yake.

 

“Alikiba ni mtu ninayemkubali, ninapenda nyimbo zake na ndiyo maana nimekuja hapa leo,” amesema Uwoya.

Mwanadada huyo pia amezungumzia kuhusiana na suala la kuzindua club  yake aliyotarajiwa kuizindua usiku wa tarehe 23, lakini amesema kuwa hakufanya hivyo kwa kuwa kuna vitu havikukamilika kwa wakati.

Comments are closed.