The House of Favourite Newspapers

Ja Rule Asema 50 Cent Anawadhalilisha Watu Wasio Weupe

 

KWA mujibu wa vyombo vya habari, wanamuziki maarufu nchini Marekani, Ja Rule na 50 Cent, ambao wamekuwa na bifu kati yao kwa karibu miaka 20, hawatafikia mwisho wa mtafaruku huo hadi “mmoja wao atoweke”.

Akiwa anasema amemtumia 50 Cent ujumbe wa mwisho, Ja Rule pamoja na kuposti picha ya 50 Cent akiwa na (Rais) Donald Trump, amempuuza mwanamuziki huyo akisema kwamba pamoja na kuwa na wafuasi milioni 20 bado hajawaonyesha kitu chochote cha maana na kwamba hata hakuwachochea ili wampigie kura Trump, badala yake anajikita katika kuwadhalilisha watu wengine ambao si Wazungu.

Moja ya vilele vya bifu lao, ni wiki kadhaa zilizopita ambapo 50 Cent aliamua kununua tiketi zipatazo 200 za kwenye shoo iliyokuwa imepangwa kufanywa na Ja Rule kwa makusudi kwamba ionekane shoo hiyo haikuingiza watu wengi.

Image result for ja rule

Comments are closed.