The House of Favourite Newspapers

Jay Z Ageukia Biashara ya Bangi

MSANII nguli wa Hip hop duniani kutoka Marekani, Jay Z amepata shavu kutoka kampuni kubwa ya utengenezaji na uzalishaji wa bangi iitwayo Caliva.

 

Jay Z amepewa nafasi ya kuwa mkurugenzi mkuu wa mipango na mikakati wa kampuni hiyo , na ameingia ubia huo wa kufanya nao kazi kwa mwaka mmoja.

 

Katika nafasi hiyo Jay Z atakuwa anasaidia masuala ya ubunifu, maamuzi , juhudi za ufikiaji malengo na mikakati. Pia atakuwa ana dili na haki za kijamii kwenye mambo ya kuhahalilsha bangi, ikiwa pamoja na utetezi, mafunzo ya kazi, kuajiri wafanya kazi, na kufanya kazi kwa maendeleo.

 

“We want to create something amazing, have fun in the process, do good and bring people along the way,” Alisema Jay Z akimaanisha kuwa, anataka afanye kazi kwa usahihi katika ngazi za juu, akitumia uwezo wake wote katika sekta hii ya biashara ya bangi, jitihada bora za kitaalamu katika kuiendesha, na kubuni kitu cha kushangaza, na kufanya vizuri ili kuleta watu katika njia sahihi.

Comments are closed.