Jean Ahoua Atingisha Simba, Kaizer Chiefs Wamnyatia kwa Karibu
MTAMBO wa mabao ndani ya kikosi cha Simba SC kinachonolewa na Kocha Mkuu, Fadlu Davids huenda ukachomolewa na matajiri wa Afrika Kusini ambao wanahitaji saini yake kwa ukaribu.
Ni Jean Ahoua kiungo mshambuliaji wa Simba SC chaguo la kwanza la Fadlu kwenye mechi za ushindani ndani ya msimu wa 2024/25.
Ahoua nim tambo wa mabao akiwa na uwezo kwenye kufunga na kutoa pasi za mabao akiingia kwenye orodha ya wakali wa mapigo huru.
Katika mabao 15 aliyofunga mguu wake wenye nguvu ni ule wa kulia akiwa kafunga mabao 14 na kwa pigo la kichwa alifunga bao moja kwenye mchezo dhidi ya Pamba Jiji alipotumia pasi ya Ellie Mpanzu.
Kwenye mchezo huo Ahoua alifunga hat trick yake ya kwanza akiwa na uzi wa Simba SC ambapo alichaguliwa kuwa mchezaji bora Simba SC iliposepa na pointi tatu mazima katika mchezo wa ligi.
Taarifa zinaeleza kuwa mabosi kutoka Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini wanamfuatilia kwa ukaribu kiungo huyo ambaye amehusika katika mabao 23 ndani ya ligi namba nne kwa ubora kati ya 63 yaliyofungwa na timu hiyo kwenye ligi namba nne kwa ubora Afrika.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu itazinduliwa rasmi Julai 24 2025 usipange kukosa.