The House of Favourite Newspapers

Joh Makini Akamilisha ‘Project’ Yake Na Chidinma

0

Joh-makini.jpgOmary Mdose, Dar es Salaam

MKALI wa Muziki wa Hop Hop Bongo, Joh Makini amefunguka kuwa tayari amekamilisha ‘project’ yake aliyofanya na msanii wa kike kutoka Nigeria, Chidinma Ekile.

Joh Makini anayeunda Kundi la Weusi, amefunguka kuwa kuanzia Jumatatu ya wiki ijayo atakuwa tayari ameachia project yake hiyo ambayo inakwenda kwa jina la Perfect Kombo.

Chidinma Ekile.“Baada ya G Nako kufanya ngoma na Nikki wa Pili inayoitwa Arosto, sasa ni zamu yangu kusikika na Jumatatu ijayo natarajia kutambulisha ngoma yangu ya Perfect Kombo, niliyofanya na mdada kutoka Nigeria, Chidinma.

“Mbali na hayo, kazi za kundi zinaendelea kama kawaida na endapo mambo yakikaa sawa basi tutafanya kitu kipya cha pamoja, kikubwa mashabiki wetu wazidi kutusapoti kwa kila hali,” alisema Joh Makini.

Leave A Reply