The House of Favourite Newspapers

JUICE KINGDOM YAANDIKA HISTORIA!

UZINDUZI wa vinywaji vya Juice Kingdom tawi la Tabata- Segerea umeandika historia ya aina yake kwa kukusanya umati mkubwa wa watu ambao walifika na kufurahia ladha mbalimbali za juisi hizo zenye ladha ya kipekee.

 

Uzinduzi huo ulifanyika Ijumaa iliyopita ambapo wakazi wa Segerea na maeneo ya jirani, kwa mara ya kwanza waliweza kuionja juisi ya Kingdom pamoja na vinywaji vingine.

“Yani tumeinjoi tunawashukuru sana Juice Kingdom kwa kutuletea vinywaji hivi baridi, vyakula vya kumwaga kwa kweli huu ni zaidi ya uzinduzi wa juisi,” alisema Juma Suku, mkazi wa Tabata Segerea.

Mbali na watu kufurahia juisi pamoja na vyakula, siku hiyo watu waliweza kupata nafasi ya kuwashuhudia wasanii mbalimbali wa Bongo Fleva na Bongo Movies.

Kwa upande wa Bongo Movies, Kulwa Kikumba ‘Dude’, Blandina Chagula ‘Johari’ na Ndumbangwe Misayo ‘Thea’ waliweza ‘ku-show love’ na mashabiki wao huku wakinywa juisi mbalimbali za Kingdom.

“Ni juisi ambazo kwa kweli sijawahi ona mahali popote Bongo. Sisi tunakunywa juisi mbalimbali lakini hii ni tamu, haichoshi tangu nimefika hapa nakunywa tu,” alisema Johari.

Wasanii wa Bongo Fleva waliotumbuiza siku hiyo na kupata shangwe kubwa ni pamoja na Young Dee, Dogo Janja na Q Boy Msafi.

Mkurugenzi wa Juice Kingdom, Zabron Julius alisema burudani kwa upande wa Tabata-Segerea ndio kwanza inaanza hivyo mashabiki vitu vyenye ubora wafike Stendi ya Segerea kuburudika.

Alisema, tofauti na matawi yake mengine yaliyopo katika kona mbalimbali za jijini Dar, tawi hilo la Tabata- Segerea lina nyama choma, baga, kuku na vyakula mbalimbali pamoja na bia!

 

“Yani mteja atachagua yeye tu kama amekuja na wenzake ambao pengine wanatumia bia, yeye anatumia juisi basi chaguo ni lake,” alisema Zabron.

Akiizungumzia juisi, Zabron alisema juisi wanavyoitengeneza ina viwango vya hali ya juu kwani hawachanganyi na kemikali ya aina yoyote.

“Juisi yetu ni nzuri, hatuchanganyi na kemikali ya aina yoyote na katika vituo vyetu tunazingatia usafi wa hali ya juu,” alisema Zabron.

Alisema ukifika kwenye vituo vyao, utapokelewa na wahudumu nadhifu, wachangamfu kiasi cha kukufanya ujisikie upo nyumbani.

Alisema juisi hizo zinapatikana kwa ukubwa na bei tofauti hivyo mteja kujinunulia kulingana na saizi anayoitaka.

Stori: Mwandishi Wetu

Comments are closed.