The House of Favourite Newspapers

Kabangu: Nikicheza na Chama, Luis Nitafunga Sana

0

MSHAMBULIAJI wa DC Motema Pembe ya DR Congo, Kadima Kabangu, amesema ubora walionao viungo wa Simba wakiongozwa na Clatous Chama na Luis Miquissone, utamfanya afunge mabao mengi iwapo atatua ndani ya kikosi hicho msimu ujao.

 

Kabangu ndani ya msimu huu wa Ligi kuu ya DR Congo akiwa na Motema Pembe, amefanikiwa kufunga mabao 9 na kutoa asisti 4 katika michezo 16, huku akifanikiwa kufunga mabao 3 katika michezo minne ya Kombe la Shirikisho Afrika.

 

Mshambuliaji huyo ameweka wazi kuwa  tayari amewasiliana na Kocha wa Simba, Didier Gomes kwa ajili ya kujiunga na timu hiyo.

Akizungumza na Spoti Xtra, Kabangu alisema: “Simba wana viungo wazuri wa kutengeneza mabao kama Chama, Luis na Bwalya (Rally), hivyo naamini kupitia wao nitafunga mabao mengi sana kama nitafanikiwa kukamilisha usajili wangu wa kujiunga na Simba katika siku zijazo.

 

“Ligi ya Tanzania nimeifuatilia na bado naendelea kuifuatilia, ni ligi nzuri na yenye ushindani mkubwa, unatakiwa kujituma kila siku ili uweze kufanikiwa kufunga kama ukiwa mshambuliaji, binafsi nimejiandaa kwa kupambana.”

STORI: MARCO MZUMBE, Dar

Leave A Reply