The House of Favourite Newspapers

Kagere Awaonya Azam FC

MSHAMBULIAJI wa Simba, Mnyarwanda, Meddie Kagere amefunguka kuwa atahakikisha anaanza kufunga mabao ya kutosha katika mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Azam FC kabla ya kuhamishia nguvu zake katika Ligi Kuu Bara.

 

Kagere ametoa kauli hiyo kuelekea mchezo huo wa Ngao ya Jamii unaotarajiwa kupigwa kesho Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar, huku mshambualiaji huyo akiwa na rekodi ya kufunga mabao 23 katika Ligi Kuu Bara msimu uliopita.

Akizungumza na Championi Ijumaa, Kagere alisema kuwa amejipanga vizuri kuhakikisha anafunga mabao ya kutosha katika mchezo huo kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu Bara kwa lengo la kutaka kuendeleza rekodi yake ya mabao.

 

“Unajua Azam siyo timu rahisi, wana timu nzuri ambayo ina uwezo wa kutoa ushindani mkubwa lakini kwangu nataka iwe sehemu ya maandalizi ya kuelekea katika ligi kuu, ninachokiangalia ni kuona jinsi gani nafikia rekodi ya msimu uliopita,” alisema Kagere.

‘MAHAKAMA’ YAMKATAA DISMAS wa YANGA / Mashabiki Watakiwa Kufanya Hiki

Comments are closed.