KAJALA hajawahi kumtamani mwingine

WAKATI wengine wakitamani kuwa kama Beyonce au Rihanna, kwa mwanamama seksi kunako Bongo Muvi, Kajala Masanja ‘Kay’ hataki kuwa kama mtu yeyote duniani kwani anajikubali kinoma. Akizungumza na Gazeti la Ijumaa Wikienda, Kajala alisema watu wengi wanatamani kuwa kama wengine, mwisho wa siku wanajisahau kabisa hata wao wenyewe, jambo ambalo hataki kulisikia.

“Tangu nikiwa mdogo sikupenda kuwa kama mtu mwingine na nilikuwa na tabia tofauti. Pia huwa ninakwazika nikiona mtu akitamani kuwa mtu mwingine maana mimi sipendi kabisa,” alisema Kajala.


Loading...

Toa comment