The House of Favourite Newspapers

Kane atakiwa kusepa Spurs

MSHAMB-ULIAJI wa Tottenham Hotspur, Harry Kane ametakiwa kuihama timu hiyo na kutafuta timu nyingine kama anataka kushinda mataji makubwa katika maisha yake ya soka.

Msimu uliopita, Kane ilibaki kidogo abebe ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, lakini timu yake ikapoteza mchezo wa fainali mbele ya Liverpool. Tangu 2009, Kane alipoanza kucheza timu ya wakubwa ya Spurs, hajashinda taji lolote.

Rio Ferdinand ambaye ni beki wa zamani wa Manchester United aliyeshinda mataji sita ya Premier na mawili ya Ligi ya Mabingwa Ulaya akiwa na kikosi hicho, amesema Kane anapaswa kuondoka Spurs kama anataka kutimiza ndoto za kutwaa mataji makubwa.

“Anakaa kwenye timu ili awe nani? Ashinde mataji au kuonekana ni mchezaji muhimu kikosini? Ukiangalia bado umri wake unaruhusu, akiwa na miaka 26 anaweza kufanya maamuzi na kwenda sehemu nyingine ambapo atakuwa na uhakika wa kushinda mataji,” alisema Ferdinand.

LONDON, ENGLAND

 

Comments are closed.