The House of Favourite Newspapers

KANE YUPO KAMILI KUIVAA LIVERPOOL

Harry Kane

STRAIKA tegemeo wa Tottenham, Harry Kane amesema yupo fiti kuivaa Liverpool kwenye mechi ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya itakayopigwa Jumamosi hii kwenye Uwanja wa Wanda Metropolitano mjini Madrid, Hispania.

 

Hatua hiyo inaongeza matumaini ya Tottenham kwenye mchezo huo wa fainali kutokana na ukali wa staa huyo katika kupachika mabao. Kane amekuwa nje ya uwanja tangu Aprili, mwaka huu wakati alipoumia kwenye mechi ya kwanza ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Manchester City.

 

Aliumia enka kwenye mchezo huo, ambapo kutokana na majeraha hayo kulikuwa na wasiwasi kuwa huenda atarudi uwanjani msimu ujao. Katika kipindi ambacho amekuwa hayupo, timu yake imewasha ngaza wengi kwa kutinga fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu.

 

Pia imekamata nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi Kuu England msimu wa 2018/19 uliomalizika hivi karibuni. Kane ni tegemeo la ufungaji la Tottenham, ambapo msimu huu alicheza mechi 39 na kupa chika mabao 24. Kitendo cha Kane kurudi uwanjani kutaongeza uhai wa fowadi ya Tottenham, ambayo katika siku za karibuni imekuwa inawategemea zaidi Heung-min Son na Lucas Moura

Comments are closed.