The House of Favourite Newspapers

Kenya: Baba Aua Mwanaye Kwa Kumsumbua Usingizini

0

Wapelelezi kutoka Idara ya Makosa ya Jinai (DCI) wamefichua kwamba wamemkamata mzee wa miaka 73, James Tarus, kwa kumuua mwanae.

Kijana huyo ambaye alikuwa mlevi alielekea chumbani kwa baba yake na kujaribu kumuamsha kwa kunyanyua kitanda jambo ambalo lilimkasirisha sana mzee huyo.

Babaake kwa hasira, alichukua kipande cha mbao akampiga na kumfunga kwa kamba shingoni na kisha kwenye kochi.

“Mwathiriwa ambaye alikuwa amekunywa chupa kadhaa alielekea nyumbani kisha hadi chumbani mwa babake akaanza kumuamsha huku akinyanyua kitanda.

Akiwa amewaka kwa hasira, mzee huyo alimpasua kichwa mwanawe kwa kutumia mbao iliyokuwa karibu, kabla ya kumfunga kwa kamba shingoni na kidha kwenye kochi,” DCI aliripoti.

DCI ilisema chifu wa eneo hilo na wananchi walifika eneo la tukio na kumkuta kijana huyo akiwa amefungwa kwenye sofa na tayari akiwa amekata kamba. Alikuwa ameaga dunia kutokana na majeraha aliyopewa na babaake, ambaye alikamatwa mara moja.

Leave A Reply