The House of Favourite Newspapers

Kigogo TRA, Miss Tz Wafutiwa Shtaka la Utakatishaji Fedha

0
1-4-768x432Kamishna Mkuu Mstaafu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Harry Kitilya (katikati) sambamba na waliokuwa wafanyakazi wa Benki ya StanBic Tanzania, Sioi Sumari (kushoto) na Shose Sinare (kulia) wakiwa Mahakama ya Kisutu.
 Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kisutu jijini Dar es Salaam, leo imefuta shtaka la utakatishaji fedha (money laundering) lililokuwa likimkabili Kamishna Mkuu Mstaafu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Harry Kitilya sambamba na waliokuwa wafanyakazi wa Benki ya StanBic Tanzania, Sioi Sumari na Shose Sinare.
Awali watatu hao walikuwa wamenyimwa dhamana. Kutokana na uamuzi huo, mawakili wao sasa wanaweza kuwaombea dhamana.

April 1, 2016 Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) iliwapandisha kizimbani aliyekuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania ‘TRA’ Harry Kitilya, mshindi wa taji la Miss Tanzania 1996 ambaye pia alikuwa Afisa Mwandamizi wa Benki ya Stanibic, Tawi la Tanzania, Bi. Shose Sinare pamoja na Sioi Solomoni kwa tuhuma mbalimbali zikiwemo za kula njama kutenda kosa pamoja, kughushi nyaraka na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu ambapo watuhumiwa walijipatia fedha kiasi cha Dola za Marekani milioni 6, mwezi Machi mwaka 2013, ili kufanikisha mkopo kutoka Benki ya Stanbic ya Jijini London mkopo ambao ulipitia benki ya Stanbic tawi la Tanzania..

Kesi hiyo ilipangwa kuendelea tena April 22, 2016 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu jijini Dar es Salaam ambapo siku hiyo kesi iliahirishwa na Hakimu Mkazi Emillius Mchauru kwa sababu hakimu hajakamilisha uandikaji wa uamuzi wa kuondoa shitaka la utakatishaji fedha linalowakabili washtakiwa wote watatu.

Hakimu Emillius Mchauru aliipanga kesi hiyo kuendelea kusikilizwa tena leo April 27, 2016 ambapo maamuzi ya kufuta shtaka la utakatishaji wa fedha limefanyika.

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), iliwafikisha mahakamani watatu hao April 1, kwa makosa ya:- Kula njama na kujipatia kwa udanganyifu kinyume na kifungu Na. 384 cha Kanuni ya Adhabu (Cap 16 R.E. 2002) ; Kughushi kinyume na kifungu Na. 333,335 (a) na 337 cha Kanuni ya Adhabu (Cap 16 R.E 2002) ; Utakatishaji wa fedha haramu kinyume na kifungu Na. 12 (a) 13 (a) cha Sheria ya ya Utakatishaji fedha Na. 12 ya Mwaka 2006 ‘Anti- Money Laundering Act’.

Leave A Reply