The House of Favourite Newspapers

KIJANA ALIYEMWOKOA MTOTO, AJIUNGA NA JESHI UFARANSA – Pichaz

KIJANA shujaa mhamiaji kutoka nchini Mali, Mamoudou Gassama aliyemwokoa mtoto aliyekuwa amening’inia kwenye kibaraza cha ghorofa ya nne katika jengo refu jijini Paris, Ufaransa tayari amejiunga na Jeshi la Zima Moto na Uokoaji la Ufaransa, baada ya kupewa ajira hiyo na Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron

Mamoudou alipanda jengo hilo refu bila kutumia vifaa vyovyote huku akishangiliwa na watu waliokuwa wamekusanyika nje ya jengo hilo, hadi kufanikisha kumfikia mtoto huyo wa kiume mwenye umri wa miaka minne na kumuokoa.

Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron alimualika kijana huyo Ikulu na kuzungumza naye, kisha akampa cheti maalum cha kutambua ushujaa wake na kuamuru apewe uraia wa Ufaransa baada ya kusikia jinsi alivyohangaika kuingia nchini humo.

 

Pia, Rais Macron alimpatia kazi Mamoudou katika Jeshi la Zima moto la Ufaransa, pia amemtunukia medali ya kipekee ya ushujaa kijana huyo na kuwataka raia wote kuiga mfano wake.

Aidha, Rais wa Mali, Ibrahim Boubacar Keïta alimtaka kijana huyo kurejea nyumbani kwao nchini Mali kwani amemwandalia kazi Jeshini, lakini ameshangaza wengi baada ya kuamua kuitikia ombi la rais wa Ufaransa na Kujiunga na jeshi la Zima Moto na Uokoaji.

Comments are closed.