The House of Favourite Newspapers

KIKI YA UWOYA, DOGO JANJA YAFIKA MWISHO

Irene Uwoya

WAFUATILIAJI wa habari za mastaa Bongo, watakumbuka wakati ule mastaa wa Bongo, Irene Uwoya na mwenziye Abdulaziz Chende ‘Dogo Janja’ walipodai kuwa wamefunga ndoa ya kiislam baada ya Uwoya kusilimu na kuitwa jina la kiislam la Sheila. Ni habari ambayo iliwashitua wengi, wapo walioamini na kusema mapenzi hayaangalii umri lakini wapo waliosema no! Uwoya hawezi kukubali kuolewa na Dogo Janja. Kuna waliosema ni filamu na kuna waliodai ni kiki tu!

Waandishi wa Global Publishers walifanya utafiti na kubaini kuwa, hakukuwa na ndoa bali ni fiksi tu. Tukaandika habari nyingi tu kuonesha kuwa wawili hao walifanya hivyo ili kutafuta kiki katika masuala yao ya sanaa! Hata pale tulipoongea na wahusika hao na kusema wamefunga ndoa, chini ya habari zetu tulionesha msimamo wetu wa kwamba hatuamini uwepo wa ndoa hiyo.

Ni takribani miezi 10 imepita, leo hii tunaona waziwazi kwamba wawili hao wameshamwagana ‘kisela’. Hii inadhihirisha kuwa, ile kiki yao imefika mwisho! Haihitaji miwani ya macho wala tochi kufahamu kuwa wawili hao imebaki historia kwani wanaowafuatilia watakuwa wanafahamu wazi nini kinaendelea.

Gumzo la wawili hao kumwagana lilianza mapema wiki hii baada ya Dogo Janja kukimbizwa hospitali kwa sababu ya matatizo ya kifua na kushindwa kupumua vizuri, kisha Uwoya kutoonesha kumjali. Dogo Janja mara kwa mara amekuwa akikinga kifua kwamba bado yupo vizuri na ‘mkewe’ lakini Uwoya amekuwa hazungumzii suala hilo na akilipuka anatoa majibu yanayoonyesha kwamba hakuna tena ndoa kati yao.Related image

TUJIKUMBUSHE ZENGWE LA NDOA YAO!

Ukweli ni kwamba ndoa ya wawili hawa ilianza kama skendo. Ilianza kwa picha kusambaa mitandaoni hasa kwenye Mtandao wa Kijamii wa Instagram zikiwaonyesha wakifunga ndoa. Penzi likaonekana kushamiri huko pia. Wawili hao walipostiana kwa zamu wakionyeshana mapenzi motomoto na namna kila mmoja anavyomjali mwenziye.

Lakini ukijaribu kufuatilia utagundua toka mwezi Mei, Dogo Janja ndiye aliyeonekana kujali zaidi kumposti Instagram Uwoya, Uwoya hana ‘time’ kabisa. Toka Mei 4, mpaka juzi Jumanne, Dogo Janja kamposti Uwoya mara tisa huku akimuandikia ujumbe mbalimbali wa kimahaba, lakini ujumbe wa mwisho unaonesha wazi mambo hayako poa. Dogo Janja aliposti picha ya Uwoya na kuandika; Bado nina imani yatapita!

UWOYA AMTOSA!

Huku Dogo Janja akionyesha kwamba bado ana imani juu ya ‘ndoa’ yake na Uwoya, mwanadada huyo yeye anaonyesha wazi amemmwaga. Kwanza ukifuatilia toka mwezi Mei, Uwoya hajamposti kabisa ‘dairekti’ Dogo Janja. Mei 26, aliposti picha ya katuni ikimuonyesha yeye na Dogo Janja wakiwa wazee kisha akaweka ‘imeji’ za kucheka.

Hakuposti tena kitu chochote kuhusu Dogo Janja mpaka Juni 29, alipoposti wimbo wa Banana ndio aliposti kava la wimbo huo na Juni 30, aliposti kipande cha video ya wimbo huo wa Banana.Image result for irene uwoya na dogo janja

POSTI TATA!

Posti tata zimeanza Septemba 17 kwenye siku ya kuzaliwa ya Dogo Janja, saa chache tu baada ya mkali huyo wa Bongo Fleva kuzidiwa na kukimbizwa hospitali. Uwoya aliposti Instagram ujumbe huu; “Happy birthday kiboko yao…MUNGU akupe umri mrefu…ila ndiyo kama vile nilivyokwambia.”Related image

Komenti zilimiminika watu wakimshangaa Uwoya kwa kuamua kuposti ujumbe huo mwenziye akipumulia oksijeni hospitali. Uwoya akaposti ujumbe mwingine uliosomeka kwamba; “Kila unachosikia kuhusu mimi tafadhali amini, sina muda wa kujielezea mwenyewe, unaweza kuongeza lolote kama unapenda…”

Ujumbe huu nao ulifanya watu watoke mapovu. Watu wakakomenti chini ya posti yake moja kwamba dogo huyo kutoka Arusha atapoteza uhai, Uwoya akaibuka na kudai watu walimshauri atafute saizi yake na aachane na Dogo Janja, huo ni ushauri alioamua kuufanyia kazi.

Kama huamini hakuna ndoa tena subiri ‘press!’ Kinachoonekana wazi hakuna ‘ndoa’ tena kati ya wawili hao. Uwoya kusema wazi amemwaga Dogo Janja na kutafuta saizi yake, ukipima pia mwenendo wao miezi mitatu iliyopita unaona wazi ‘ndoa’ yao imeshaingia shubiri.

Lakini kwa ambao hawaamini kwamba hakuna tena ndoa, wasubiri mkutano wa waandishi ‘press’, pengine ataamua kulizungumzia hili, kama sivyo ninaamini ndani ya siku chache kila kitu kitakuwa wazi! Hata hivyo, sisi bado tunaendelea kuamini kuwa, hakukuwa na ndoa bali ilikuwa ni kiki tu na kiki yenyewe ndiyo imefika mwisho.

Makala: Boniphace Ngumije

Comments are closed.