The House of Favourite Newspapers

Kim, Kanye Wamaliza Uvumi wa Talaka kwa Picha ya Krismasi

kanye

Zile tetesi za chini kwa chini kwamba ndoa ya mastaa wawili wakubwa nchini Marekani, Kim Kardashian na Kanye West ipo kwenye hatihati ya kuvunjika kutokana na mgogoro mkubwa unaoendelea kati ya wanandoa hao, ni kama zimezimwa baada wawili hao, mapema jana kupost picha mtandaoni ya kuwatakia heri ya Krismasi na Mwaka Mpya mashabiki wao.

Picha hiyo inaonesha ilipigwa nyumbani kwa mama yake Kardashian, ambapo wawili hao wanaonekana wakiwa wamesimama pamoja, kila mmoja akiwa amembeba mtoto mmoja, Kanye akiwa amembeba North na Kim akiwa amembeba Saint.

Hii ni mara ya kwanza kwa wanandoa hao kupiga picha ya pamoja, tangu Kim alipovamiwa na vibaka mwezi Oktoba, na kuporwa vitu mbalimbali. Ndani ya muda mfupi tu tangu kupostiwa kwa picha hiyo, mashabiki wengi walii-like na kutoa comments zao, wengine wakiwaponda kwamba walikuwa wakiigiza na wengine wakiwapongeza kwa kuyamaliza matatizo kati yao.

 

Mjane wa Mtikila Avaa Viatu vya Mumewe, Asisitiza Mumewe Kauawa, Ataja Sababu

Comments are closed.