Kisa Yanga, Simba Wamficha Chama

UONGOZI wa Simba umetamba kuwa mipango yao ya usajili inakwenda vizuri katika dirisha dogo wakipanga kufanya kwa siri huku wakitamka kiungo wao wa zamani anayekipiga RS Berkane ya nchini Morocco, Clatous Chama huenda akawa mmoja wao.


Kauli hiyo wameitoa mara baada ya
kuwepo tetesi za Yanga kuwepo katika mipango ya kuwania saini ya Chama
katika usajili huo wa dirisha dogo
ambalo limefunguliwa juzi.

 

Inaelezwa kuwa kiungo huyo ameomba mwenyewe mkataba wake kuvunjwa kutokana na kutokuwa na furaha na timu hiyo tangu amejiunga nayo katika msimu huu.

 

Akizungumza na Championi Jumamosi, Kaimu Ofisa Habari wa Simba, Ally Shatry alisema kuwa ngumu kwao kwa hivi sasa kuweka wazi usajili wao dirisha likiwa limefunguliwa juzi Alhamisi.


Shatry alisema kuwa, watatangaza
na kuweka wazi mipango yao ya usajili mara baada ya kila kitu kukamilika kwa kila mchezaji aliyekuwepo katika mipango yao.


Aliongeza kuwa Simba ni
timu kubwa, akijulikana mchezaji wanayemuhitaji ni lazima klabu nyingine
zinahitaji saini yake, hivyo wataendelea
na usajili wao kimyakimya.


“Niwaondoe hofu Wanasimba kuwa
kila kitu kinachohusiana na usajili wetu kinakwenda vizuri kwa hivi sasa
tunafanya siri.


“Kila kitu kitakapokamilika, basi
tutaweka wazi katika usajili wetu wa dirisha dogo, lakini kwa hivi sasa
uongozi unaendelea na mipango yake ya
usajili kwa wachezaji wa ndani na nje ya nchi.

 

“Na kuhusiana na Chama huenda akawa ni kati ya wachezaji tutakaowasajili, lakini kikubwa tutafanya
usajili wetu kutokana na mahitaji ya
kocha wetu Pablo,” alisema Shatry.

Stori: Wilbert Molandi, Dar es Salaam705
SWALI LA LEO

Kupanda Kwa Bei ya Mafuta Nchini, Nini Kifanyike Kupunguza Bei?
Toa comment