The House of Favourite Newspapers

Kisutu: Watathmini wa Almasi wa Serikali Wafikishwa Mahakamani

0
Watathmini wa serikali wa almasi, Archard Kalugendo na Edward Rweyemamu (katikati) kutoka Wizara ya Nishati na Madini wakishuka ngazi.

 

Watathmini wa serikali wa almasi, Archard Kalugendo na Edward Rweyemamu kutoka Wizara ya Nishati na Madini wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashitaka ya kusababisha serikali hasara ya Sh bilioni 2. 4.

Washitakiwa hao ambao ni Mkurugenzi wa Tathmini na Mthamini wa madini, wamesomewa mashitaka mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Respicious Mwijage na Wakili wa serikali, Paul Kadushi.

Archard Kalugendo

Kadushi amedai kuwa kati ya Agosti 25 na 31, mwaka huu maeneo ya Dar es Salaam na Shinyanga wakiwa watathmini wa serikali walisababisha hasara ya dola za Marekani 1,118,291.43 sawa na Sh bilioni 2,486,396,982.

Kadushi amedai upelelezi wa shauri hilo haujakamilika wanaomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.

Hakimu Mwijage amesema washitakiwa hawatakiwi kujibu chochote hadi Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) atakapoamua iendelee hapo mahakamani au la. Pia amesema masuala ya dhamana sheria kama zilivyo inafikiriwa na Mahakama Kuu ya Tanzania hivyo mawakili watafuatilia.

Habari na Denis Mtima

Breaking News: Polisi, TCRA Wafunguka Kuhusu Uhalifu Mitandaoni

Leave A Reply