The House of Favourite Newspapers

Kiungo Fundi wa Al Hilal Mambo Safi Yanga Injinia Hersi Said Afunguka

0
Kiungo fundi wa Al Hilal ya Sudan, Fabrice Ngoma.

RASMI imebainika klabu ya Yanga imeanza rasmi mazungumzo ya kumsajili kiungo fundi wa Al Hilal ya Sudan, Fabrice Ngoma ambaye tayari uongozi wake umeomba kuondoka ndani ya kikosi hicho.

Mastaa wa kimataifa wa Klabu ya Al Hilal wametimka Sudan kutokana na vita inayoendelea nchini humo na kusababisha ligi kusimama.

Yanga tayari kupitia kwa Rais wa Yanga, Injinia Hersi Said ameweka wazi mipango ya usajili wa Yanga kwa ajili ya msimu ujao ambapo amesema kuwa ripoti kutoka kwa benchi la ufundi la timu hiyo chini ya Kocha Nassredine Nabi inahitaji kuongeza majembe mapya na kupunguza wachezaji wengine.

Taarifa ambazo limezipata Championi Jumatano kutoka chanzo cha kuaminika zinaeleza juu ya Yanga kumtengea mkataba wa miaka miwili kiungo huyo huku mazungumzo yakiwa yanaendelea baina ya pande zote mbili.

Chanzo cha ndani pia kutoka DR Congo kimelipa taarifa Gazeti la Championi Jumatano juu ya Yanga tayari kuanza mazungumzo ya kumsajili Fabrice Ngoma ambapo tayari wameshawasilisha ofa ya mkataba wa miaka 2 kumpata kiungo huyo ambaye kupitia uongozi wake umeweka wazi kuhitaji kuondoka Sudan kutokana na hali ilivyo.

“Uongozi wa Al Hilal upo kwenye wakati mgumu sana hiyo ni kutokana na hali ilivyo kwa sasa ya kiusalama nchini Sudan kuwa na machafuko hivyo wachezaji wengi sana wameomba kuondoka akiwemo Fabrice Ngoma.

“Yanga tayari wamewasilisha ofa yao ya kumtaka Fabrice Ngoma ikiwa na mkataba wa miaka 2, tayari mazungumzo yanaendelea baina ya Yanga na uongozi wa Ngoma na Al Hilal hivyo dili linaweza kukamilika muda wowote,” kilisema chanzo hiko.

Stori na Marco Mzumbe

MAPYA YAIBUKA, UGOMVI WA GIGY NA BABA LEVO WAFIKA PABAYA,MADOLALI ATIA NENO

Leave A Reply