Kocha Simba amfungia kazi Ibrahim Ajibu

MBELGIJI hataki ujinga hii ni baada ya kumfungia kazi straika wake mahiri, Ibrahim Ajibu kwa kuhakikisha anafanya mazoezi kwa ufasaha zaidi huku kocha Adel Zrane akipewa jukumu la kudili na staa huyo.

 

Habari za ndani zinadai kuwa kocha haridhishwi na jinsi nyota huyo anavyofanya mazoezi huku ikionekana kuwa amekuwa ni mvivu na hafanyi ipasavyo hivyo kwa sasa amekuwa akiangaliwa kwa ukaribu zaidi.

 

Chanzo hicho kilidai kuwa nyota huyo amekuwa akifanya mazoezi lakini si kwa bidii anayoitaka kocha kama ambavyo wanakuwa wanafanya wenzake ndiyo maana Aussems baada ya kugundua hilo amekuwa akimfuatilia kwa ukaribu zaidi na kumpa jukumu Zrane la kumfanyia kazi zaidi.

Spoti Xtra lilizungumza na kocha Aussems kuhusiana na kiwango cha nyota wake huyo mpya pamoja na wageni wengine na alifunguka hivi: “Siwezi kuzungumzia kiwango cha Ajibu kwa sasa kwanza ametoka kwenye majeruhi na pia amecheza mechi moja bado anahitaji muda atakuwa sawa.”

MARTHA MBOMA NA MUSA MATEJA, Da


Loading...

Toa comment