The House of Favourite Newspapers

KOMBE LA SIMBA LAPELEKWA MORO, SIMBA 1-1 BIASHARA TAIFA

MCHEZO wa leo uliochezwa Uwanja wa Taifa kati ya Simba na Biashara United umekamilika kwa timu zote kutoshana nguvu kwa kufungana bao 1-1.

Biashara United walianza kupachika bao dakika ya 14 kupitia kwa Innocent Edwin na Simba walisawazisha kupitia kwa Clatous Chama dk ya 17.

Sherehe za kukabidhiwa kombe leo kwa mabingwa wa Ligi Kuu Bara Simba ambazo zilipangwa kufanyika leo zimepelekwa mbele mpaka Mei 28, uwanja wa Jamhuri, Morogoro.

Simba leo walitarajiwa kukabidhiwa kombe uwanja wa Taifa imeshindikana kutokana na udhuru wa mgeni rasmi wa sherehe hizo ambaye alikuwa ni Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola.

Mchezo wa leo dhidi ya Biashara umemalizika kwa sare ya kufungana bao 1-1.

Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi, Boniphace Wambura amesema kuwa sababu kubwa iliyofanya sherehe kughairishwa ni dharula ya mgeni rasmi.

“Mgeni rasmi amekuwa na udhuru ghafla hivyo imetufanya tuipeleke mbele sherehe hii, Simba wamekubali na mipango inakwenda sawa,” amesema.

PICHA: RICHARD BUKOS NA MUSA MATEJA | GPL

Comments are closed.