Kuelekea Uzinduzi wa “Amazing Tanzania” Mawaziri Tanzania, China Wakutana
Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Dkt. Pindi Chana, amekutana na Naibu Waziri wa Utalii na Utamaduni kutoka China, Lu Yingchuan, kuelekea sherehe za jioni ya leo za miaka 60 ya Ushirikiano katika Utalii na Utamaduni kati ya nchi hizo mbili na kuahidiana ushirikiano zaidi katika sekta zao.
Kikao hicho pia kimehudhuriwa na Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma na Makatibu na Manaibu Katibu Wakuu wa Wizara hizo na wataalamu wengine.
Awali Naibu Waziri huyo kutoka China alitembelea soko la vinyago Mwenge na Makumbusho ya Taifa na kuvutiwa na sanaa na urithi wa kihistoria uliopo Tanzania.
Macho yote sasa ni jioni ya leo uzinduzi wa Meilii Tansaniya/ Amazing Tanzania.