The House of Favourite Newspapers

Kuku Hanyonyolewi Kwa Maji ya Barafu

0

HAYA haya tena jamani nimekuja miye mwenye maneno ya shombo, eti sina tofauti na harufu ya kambare, sina siri kama kitanda cha springi, ambacho wakati wa mambo yetu hasa mwanamke anapokukuruka kisawasawa, lazima majirani wapekepeke salamu watazipata na kesho kuwa gumzo la siku mtaani, upo babu wee! Sina haja ya kukusalimu leo maana umeshanivimbisha domo mi mwanakwetu! Hamu na wee imeniisha Baba Sukari.

Baba usiye na haya, baba mzebemzebe kutwa kukimbilia kutoka na watoto wadogo wasiojua mapenzi ni nini? Utalikuta baba zima ovyooo na mtoto wa shule asiyejua hata kuoga, mtoto ananuka kikwapa kama siyo maziwa, loo! Chuki chukia walaaa miye hunitishi huu moto mwingine kuuzima usije na mabua, lazima nikwambie ukweli bwana wee! Hivi mpaka leo kuna wababa wa aina hii kumbe! Haya ndo tuseme wadogo wana ladha yake, hee hee heeeiya nijichekee kwa hasira mwana we, maana nashindwa hata kulia, roho inaniuma! Utakulaje kifaranga uache kuku aliyenona?
Niwageukie na nyie watoto, vibinti vidogovidogo tena vingine vihausigeli, hivi mlishawahi kujiuliza kwa hiyo mibaba sukari kama hamtafuti magonjwa au mimba za utoto mnatafuta nini? Au mnajidanganya shughuli mnaiweza, mtamudu hayo magogo yanayopishana kuingia kiwandani. Naongea na weye mwanaizaya usiye na haya, najua ushaanza kutoa macho kama kipofu aliyebahatika kuona siku moja kwa bahati mbaya, upo? Endelea kuniangalia na kunisoma, mi nasema na wee kwa uso mpana, sikuogopi wala sijitii ubaya!

Tena usinitolee hilo tumbo kubwa kama zile gari ndogo wanazoziita bito, babu wee raha ya mechi umpate anayejua kuicheza, anayejua kupiga vyenga siyo umekaa kama lifti za kwenye maghorofa unachukuwa vitoto vidogo visivyojua hata kucheza kama feni, vitoto vilivyozoea katikati ya uwanja kukaa tu kama gogo, inahu! Utalikuta baba zima jasho linamtoka kwa kupiga ngoma huku likiimba na kucheza lenyewe, mwenzake katulia tuli akisubiri amwagiwe mzigo wako umpe chake ili awahi nyumbani kwao anapoishi na wazazi wake.

Kwa penzi kama hilo ni sawa na kumnyonyoa kuku kwa kutumia maji ya baridi, utaona ugumu wake tu! Sasa upo na mtoto mdogo sawa na mwanao hajui karibu mpenzi, hajui kulegeza macho, hajui sehemu gani unahitaji msaada wake, hajui kukupa maneno matamu yatakayokufanya uione safari fupi. Hajui kukupa pole baada ya safari ndefu zaidi ya asante baada ya kumpa chake.

Mnaweza kusema nabwabwaja kwa vile mdomo mali yangu na mdomo ni nyumba ya maneno, asikuambie mtu raha ya mapenzi umkute mwanamke anayejua kuutumia mwili, sauti na macho yake. Mmh mashalaaa wee acha tu ulikuwa wa kumpa elfu tano unampa ishirini si kwa kukuomba bali kutokana na jinsi alivyojua kukupa burudani ya kiutu uzima. Kwa leo niishie hapa mwanakwetu tukutane tena wiki ijayo. Ni mimi Anti Nasra Shangingi Mstaafu

Leave A Reply