The House of Favourite Newspapers

Maskini Lucky Vincent, Wanafunzi Wamwaga Machozi Tena!

0
Mnara Maalumu wa kumbukumbu ya wanafunzi wa Lucky Vincent waliofariki kwenye ajali.

 

Kutoka katika Shule ya Msingi, Lucky Vincent, Karatu.

Ni siku moja tangu watoto watatu, Wilson, Sadia pamoja na Doreen wawasili nchini. Watoto hao walinusurika katika ajali ya gari miezi mitatu iliyopita walipokuwa wakienda Karatu katika ziara ya masomo. leo wanakaribishwa rasmi shuleni kwao.

Watoto  wakiangua vilio.

 

Pia, mnara maalumu wa kumbukumbu ya watoto 32, walimu wawili, na dereva mmoja walioaga dunia kwenye ajali hiyo, umezinduliwa rasmi ikiwa ni ishara ya kuwaenzi na kuwakumbuka daima.

Vilio na hudhuni vilitawala shuleni hapo.

 

Wakati wa uzinduzi wa mnara, wazazi, walimu na  wanafunzi wa shule hiyo pamoja na walionusurika, wameshindwa kujizuia na kujikuta wakiangua vilio walipokuwa wakiweka mashada ya maua kwenye mnara.

Mwandishi: Edwin Lindege | GPL

Usipitwe na Matukio, Install ===>Global Publishers App

Tazama tukio zima kupitia Global TV Online

Leave A Reply