The House of Favourite Newspapers

Rais Magufuli: Siogopi Kufungwa

1
Rais Dkt. John Pombe Magufuli.

 

RAIS Dkt. John Pombe Magufuli ‘JPM’ amesema yeye kama kiongozi mkuu wa nchi haogopi vitisho vya kufungwa ama kushtakiwa vinavyotajwa na baadhi ya wanasiasa baada ya kuwashughulikia wawekezaji wanaokiuka mikataba na kuhujumu uchumi wa nchi na badala yake ataendelea kuwatetea Watanzania wanyonge ili wapate haki yao.

JPM ameyasema hayo leo wakati akiwahutubia wananchi wa Kigoma katika Uwanja wa Lake Tanganyika mjini humo.

“Hii nchi imejaa mafisadi, wamo wa CCM, Chadema, CUF, ACT, wazungu na wengine hawana chama.

“Siogopi kufungwa, kama mliniteua niwatetee, nitawatetea kwa nguvu zangu zote juu ya majizi, tumeibiwa vya kutosha, madini yetu yanachimbwa yanapelekwa nje na hatupati kitu.

“Wengine wamelipwa pesa ili kupinga tusichukue hatua dhidi ya majizi, nawaambia mimi kama rais nimejitoa kufa na kupona mpaka nihakikishe mali za Watanzania wanyonge haziibiwi na haki yao wanaipata.

“Watambue kwamba sitafungwa badala yao majizi ndiyo yatafungwa. Ilikuwa lazima tubadilishe sheria zetu hatuwezi kuendelea kuibiwa rasilimali zetu,” alisema Rais Magufuli.

 

Yaliyojiri kwenye mkutano huo.

1 Comment
  1. […] ya ‘Magufuli Baki’ iliyoanzishwa karibuni na mwanaharakati ambaye pia aliwahi kuwa mgombea ubunge wa Jimbo la […]

Leave A Reply