
Rasmi Klabu ya Yanga leo Januari 5, 2022 wamesaini mkataba wa makubaliano na Kampuni za KILINET na N-Cards kwa ajili ya kutengeneza kadi za kidigitali zitazokuwa zinatumiwa na Wanachama wa Club yetu ikiwa ni sehemu ya hatua za awali kwenye mfumo mpya wa uendeshaji, kadi moja itauzwa TZS 29,000.

“Leo imekuwa siku ya kihistoria na sasa hivi klabu ya Yanga inaenda katika mabadiliko ya kidigitali na Kilinet tumepata fursa ya kufanya kazi na Yanga kuleta teknolojia za kisasa kwa ajili ya kuliwezesha ili jambo kufanyika kikamilifu.
Jukumu la Kilinet ni kuangalia na kuzifanyia kazi michakato na mikakati ya Yanga kwa kutumia teknolojia za kisasa”- Mkurugenzi mtendaji Kilinet Mohammed Saleh