LIVERPOOL YAMTEMA STURRIDGE

LIVERPOOL imetema mastaa wake wakiwamo straika Daniel Sturridge na beki Alberto Moreno kutoka kwenye kikosi chao.

 

Pia kipa Adam Bogdan ametajwa kuachwa katika kikosi chao cha msimu ujao wa 2019/20. Katika taarifa yake, kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp alipongeza wachezaji hao kwa mchango wao katika timu ya Liverpool. “Ninawashukuru sana wachezaji hawa kwa mchango wao, kwani nilipotua Liverpool nilikuwa na wachezaji hawa kwa hiyo naelewa vizuri mchango wao,” alisema.

 

Sturridge alikuwa tishio katika kupachika mabao lakini tatizo la majeruha lilimfanya apotee katika kikosi cha kwanza. Straika huyo, ambaye aljiunga na Liverpool mwaka 2012, ameichezea Liverpool mara 160 na kupachika mabao 67.

 

Moreno, ambaye alijiunga na Liverpool mwaka 2014, alichezea timu hiyo mara 90 na kupachika mabao matatu. Bogdan aliichezea Liverpool mara sita tu tangu asajiliwe kutoka Bolton mwaka 2015.


Loading...

Toa comment