The House of Favourite Newspapers

Lowassa Ajiondoa Monduli

KADA wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Fred Lowassa,  jana Agosti 15 amejiondoa kwenye kinyang’anyiro cha wanawania kuteuliwa na chama hicho kugombea ubunge Jimbo la Monduli na badala yake chama hicho kimempitisha diwani wa kata ya Lepurko, Yonas Masiaya Laizer,  kuwania ubunge wa jimbo hilo.

 

Fred, ambaye ni mtoto wa Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa alichukua fomu ya kuwania ubunge jimbo hilo wiki iliyopita baada ya aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Julius Kalanga, kujiuzulu uanachama wa Chadema na ubunge na kuhamia CCM. Kalanga ameshateuliwa na CCM kugombea ubunge wa jimbo hilo.

 

Akizungumzia uamuzi wa Fred, katibu wa Chadema mkoa wa Arusha, Amani Golugwa, alisema baada ya kushauriana, vikao vya uteuzi vilikubali kuondoa jina lake.

 

“Ni kweli nathibitisha kuwa ameomba kujitoa, kwa sasa si wakati muafaka licha ya kuwa alionesha nia awali na wananchi wengi walimuunga mkono, hivyo chama kimekubali maombi yake na kimempitisha mgombea mwingine,” amesema Golugwa.

Comments are closed.