Lulu Diva afungukia kumvuruga Tanasha!

DAR ES SALAAM: Agosti 2, mwaka huu, staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ alilazimika kukanusha habari zilizokuwa zikienea kwa kasi ya ajabu kuwa alichepuka na mrembo wa Bongo Fleva, Lulu Abbas ‘Lulu Diva’, jambo lililomtibua vilivyo mwandani wake wa sasa, Tanasha Donna Oketch.

Jinamizi hilo halikumuacha kwani hivi karibuni tena sakata jipya liliibuka kati ya Diamond au Mondi na Lulu Diva ambapo mrembo huyo anadaiwa kutaka kuvuruga ile shughuli ya Tanasha ya baby shower iliyofanyika ndani ya Hoteli ya Best Western Coral Beach iliyopo Masaki jijini Dar.

Safari hii mkanushaji siyo Mondi bali ni Lulu Diva ambaye amezungumza na gazeti hili la Ijumaa na kufunguka kuhusu ishu hiyo. Madai ya Lulu Diva yaliibuliwa na ukurasa mmoja wa udaku kwenye Mtandao wa Instagram ambapo ilidaiwa kuwa, usiku ule wa baby shower ya Tanasha, eti Lulu Diva alikuwa akiwasiliana na Mondi, jambo ambalo Tanasha alilishtukia na kumaindi ile mbaya.

Ilisemekana kuwa baada ya Lulu Diva kushindwa kuafikiana na Mondi, alituma watu wake ambao walikuwa wakilazimisha kuingia kwenye shughuli hiyo kwa nguvu na walipokataliwa ndipo wakalianzisha. Ilidaiwa kuwa, nje ya hoteli hiyo kuliibuka vurugu kubwa za watu wa Lulu Diva ambapo walipokea kipigo kizito kutoka kwa walinzi kabla ya kukimbia.

Katika mahojiano maalum na Gazeti la Ijumaa, Lulu Diva alionesha kutibuliwa na jambo hilo ambapo bila kukiri au kukanusha habari hizo, alidai kwamba ataamsha moto ambao kila mtu ataushangaa na haujawahi kusikika. “Ni nani aliniona au aliona nikiwatuma watu? Unajua kuna mambo mengi sana ninayasikia, lakini nitawahenyesha watu,” alisema Lulu Diva bila kufafanua kauli zake.


Loading...

Toa comment