The House of Favourite Newspapers

Lulu Diva: Nampenda Belle 9, nimemfanyia video

 

MSANII wa Bongo Fleva, Lulu Abbas ‘Lulu Diva’ ameweka kumpenda msanii mwenzake, Abdenego Damian ‘Belle 9’ kwa kusema alimsaidia sana wakati anatoka kimuziki.

 

Lulu anayetikisa na ngoma kibao kama Nilegeze na Ona aliyasema hayo katika mahojiano na +255 Global Radio katika kipindi cha Bongo 255 kuwa kipaji chake kilisaidiwa kwa kiasi kikubwa na Belle 9.

 

 

“Kipaji changu nilianza kukigundua mwenyewe na marafiki zangu shuleni na washkaji zangu walikuwa wakipenda kuniambia hivyo. Pili nilivyokuja rasmi kwenye muziki Belle 9 aliniambia naweza muziki.

 

“Basi tukawa tunaendelea mwisho wa siku akaniambia anaweza kunikutanisha na Barnaba. Sasa watu wasichokijua Belle 9 ndiyo alinikutanisha na Barnaba na ndiyo maana nampenda sana. Watu wanasema tu ohh Lulu yupo karibu na Belle 9 bila kujua nimetoka naye mbali sana,” alisema Lulu Diva na kuongeza;

 

Lulu Diva akisalimiana na Mhariri wa Gazeti Champion Selehe Ally Jembe

 

“Nina nyimbo zake kama mbili nimemfanyia video, siyo kwamba nimemlipia hapana nimehusika kama video vixen ikiwemo ile ya Burger Movie Selfie buree kabisa.”

 

 

Lulu amezungumza mengi, kuyapata mahojiano zaidi waweza tembelea kurasa za 255 Global Radio katika mitandao ya kijamii ya Twitter, Facebook na Instagram kisha ingia kwenye link katika Bio.

 

Unaweza pia kuyapata mahojiano kwa kuingia katika Youtube kwa kuandika Global TV Online kisha ukiingia utakutana na full ‘interview’ kwa njia ya video.

 

TAZAMA INTERVIEW VIDEO HAPA

Comments are closed.