The House of Favourite Newspapers

Lusajo Mchezaji Bora Desemba

0

KIUNGO mshambuliaji wa timu ya Namungo FC, Reliant Lusajo amechaguliwa Mchezaji Bora wa mwezi Desemba wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Kwa mujibu wa taarifa ya Idara ya Habari ya Bodi ya Ligi Kuu nchini (TPLB iliyotolewa leo, Lusajo amewashinda Saido Ntibazonkiza wa Yanga na Haji Ugando wa Coastal Union, ambapo kwa mwezi Desemba nyota huyo alifunga mabao matatu na alikuwa na kiwango kizuri uwanjani.

Pia Melsi Medo wa Coastal Union ameachaguliwa Kocha Bora wa mwezi huo wa ligi hiyo baada ya kuiongoza Coastal Union kushinda michezo mitatu na kufungwa mmoja, ikipaa katika msimamo wa ligi kutoka nafasi ya tisa hadi ya nne katika msimamo wa ligi. Medo amewashinda Pablo Franco wa Simba na Nasreddine Nabi wa Yanga.

Lusajo anakuwa mchezaji wa nne kupata tuzo msimu huu akitanguliwa na Jeremiah Juma wa Prisons (Novemba), Feisal Salum wa Yanga (Oktoba) na Vital Mayanga wa Polisi Tanzania (Septemba).

Leave A Reply